Header Ads


NCHI ZA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA (SADC) KUFANYA ZOEZI LA PAMOJA LA KIJESHI TANGA

Hassan Hashim Tanga

Nchi wanachama wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa afrika SADC zitaendesha zoezi la pamoja la kijeshi kwa ajili ya kujiandaa na kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhalifu unaoweza kutokea  ndani ya nchi hizo.

Akizungumza katika mkutano na  waandishi wa habari kiongozi wa zoezi hilo Meja jen Harison Masebo amesema nchi ya Tanzania imekuwa mwenyeji katika kutekeleza zoezi hilo la kijeshi linafanyika kila mwaka ambalo limepewa jina la operesheni Matumbawe

Amesema miongoni mwa mambo yatakayofanyika ni kuwapa askari mbinu za kiulinzi pamoja za kukabiliana na makundi ya kihalifu

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Tanga MARTIN SHIGELA amewataka wananchi kuwa na utulivu wakati wa zoezi hilo na kuondoa hofu pindi watakapo waona askari wa kigeni mitaani .

Zoezi hilo linashirikisha nchi za Tanzania, Zambia, Malawi, Zimbawe,Afrika kusini,Lesotho na Botswana

 …………………… 
MKUU WA "OPARESHENI MATUMBAWE" MEJ..JEN HARRISON MASEBO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KULIA NI MKUU WA MKOA WA TANGA MARTIN SHIGELA

BAADHI YA WAPIGANAJI KUTOKA NCHI ZA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA  SADC WAKIWA KATIKA MKUTANO NA VYOMBO VYA HABARI MKOANI TANGA



MEJ. JEN. HARRISON MASEBO AKITOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JIJINI TANGA





Add caption

No comments:

Powered by Blogger.