Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm linawashikilia watuhumiwa 325
Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm linawashikilia watuhumiwa 325 wa matukio mbali mbali ya uhalifu katika msako mkali unaoendelea jijini dsm ambapo pia jeshi hilo limepiga marufuku uuzwaji wa silaha za kienyeji barabarani yakiwemo mapanga,Visu,pinde mikuki na manati .
Kamishna wa Polisi kanda Maalum Dsm Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari amesema watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na wanaojihusisha na Unyang'anyi wa kutumia nguvu,makundi ya uvamizi katika nyumba maarufu kumi nje kumi ndani pamoja na makundi ya waporaji yayowavizia watu giza linapoingia.
Aidha Upigaji marufuku wa silaha za jadi amesema jeshi hilo limebaini zimekuwa zikitumika mara kwa mara katika matukio ya Uporaji pamoja na kuwatisha wananchi hivyo silaha hizo kuanzia sasa zinatakiwa kuuzwa maeneo maalum pamoja na muuzaji kuwa na kibali.
Aidha jeshi hilo limesema kesho linafanya maadhimisho maalum ya jeshi hilo maarufu Polisi Day katika viwanja vya leaders kinondoni ambapo wataonyesha mazoezi ya Kipolisi mbali mbali lakini pia baada ya hapo watashiriki katika zoezi la usafi katika hospitali za mwananyamala,temeke,ilala na muhimbili.

No comments: