Header Ads


WAZIRI WA MIFUGO LUHAGA MPINA AAGIZA KUVUNJWA KWA MKATABA KATI YA RANCHI YA MZERI NA KAMPUNI YA OVERLAND

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akitoa taarifa kwa waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina wakati ziara yake mkoani Tanga



Meneja uzalishaji na uendeshaji Ranchi za Taifa Kafumu Bwire akimweleza Waziri changamoto za mkataba wa ranchi ya Mzeri na kampuni ya Overland( OVENCO)ambao umeshindwa kufanya kazi ilivyokusudiwa 



Mkurugenzi wa kampuni ya overland Feisal Edha akitoa taarifa ya  uendeshaji wa ranchi hiyo ambapo kampuni hiyo ina asilimia 70 ya hisa



waziri Mpina akizungumza na waandishi kuhusu uamuzi wa kuvunja mkataba wa ranchi ya mzeri na mwekezaji 

Baadhi ya Ng'ombe wa kisasa katika ranchi ya mzeri 


kampuni ya Overland imewekeza Ng'ombe wa kisasa kwa lengo la kuibadili sekta hiyo kuondokana na ufugaji wa kizamani 

Mkurugenzi wa kampuni ya Overland Feisal Edha akizungumza na Waziri wa mifugo Luhaga Mpina kulia ni mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe


Baadhi ya wafanyakazi wa ranchi ya mzeri inayomilikiwa kwa asilimia 70 na kampuni ya overland wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mifugo Luhaga Mpina





Mkurugenzi wa Kampuni  Stage farm fabian Shempemba akimweleza Waziri Mpina ufugaji wa samaki katika moja ya vitalu vya  ranchi ya mzeri

Moja ya mabwawa ya ufugaji samaki katika moja ya vitalu vya ranchi ya Mzeri 



Baadhi ya ngo'mbe walionenepeshwa kwa ajili ya nyama 

Waziri wa Mifugo na uvuvi  Luhaga Mpina Akiangalia taarifa ya kampuni ya stage farm ambayo ni mwekezaji katika vitalu vya ranchi hiyo


Hassan Hashim Handeni.

Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameagiza kuvunjwa kwa mkataba kati ya ranchi ya Mzeri na Kampuni ya Overland ambao ilianzisha  kampuni ya OVENCO kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza na kuitaka Narco kutengeneza mkataba mpya utakaozingatia maslahi ya taifa.

Agizo hilo amelitoa wakati wa ziara yake katika ranchi Mzeri iliyopo wilayani Handeni ambapo baada ya kupokea taarifa amebaini kutokamilika kwa uundwaji wa bodi kampuni OVENCO na kuiacha kampuni ya overland yenye 70% ya hisa kufanya shughuli zake bila usimamizi wa pamoja.

Amesema  Mkataba uliopo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka miwili uvunjwe ifikapo disemba 31 mwaka huu na kutengeneza mpya ambao utaainisha thamani ya uwekezaji  na ukubwa wa eneo kulingana na mahitaji ya mwekezaji badala ya kuhodhi ardhi kubwa bila ya kuendelezwa.
..
Aidha Waziri Mpina amesema pamoja na kasoro zilizopo kwenye mkataba wa uanzishwaji wa Ovenco ameridhishwa na juhudi za mwekezaji  katika kuinua sekta ya mifugo na kwamba wakati mkataba mpya ukiandaliwa maslahi ya mwekezaji huyo yatalindwa.

Akizungumzia hatua hiyo ya waziri meneja uzalishaji uendeshaji ranchi za taifa Bwire Kafumu  amesema Narco itafanya uhakiki wa thamani halisi wa mali zilizopo na kuishauri serikali.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya overland Feisal Edha amesema ameridhishwa na hatua ya waziri ambayo itatoa fursa na haki kwa pande zote

……………………….







No comments:

Powered by Blogger.