SABURIA MOHAMED SHOSI ALIYETUHUMIWA NA SWABAHA KUWA NIMUUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA
Hassan Hashim Tanga
SAKATA la mwanamke
aliyelalamika kwa Rais
Sakata la mgogoro wa
mirathi ya Mohamed Shossi ambalo lilifikishwa kwa Rais Magufuli na Bi Swabaha Mohamed wakati wa
maadhimisho ya siku ya sheria limechukua sura mpya baada mtoto wa marehemu kujitokeza
na kupinga madai yaliyotolewa na mjane huyo.
Akizungumza na vyombo vya
habari Saburia Mohamed Shosi amesema kitendo
cha mama huyo kumtangazia kwamba anauza madawa ya kulevya kimemvunjia heshima
mbele ya Rais na umma wa watanzania na kwamba anajipanga kuchukua hatua za
kisheria.
Kuhusu mgogoro wa mirathi
Saburia amekiri kuwa Swabaha alikua akimuita baba yao mjomba hata hivyo amesema hawezi kuzungumzia
suala hilo kwa sasa kwa sababu kesi hiyo bado iko mahakamani.
Katika kilele cha maadhimisho
ya siku ya sheria yaliyofanyika tarehe
2/2/2017 Swabaha alijitokeza mbele ya
Rais akiwa na bango na kuondolewa na walinzi wa usalama ambapo baadae
Rais aliagiza arejeshwe ndipo alipo muueleza rais kwamba anazungushwa kupata
haki yake ya mirathi ya mume wake.
………………………………………
No comments: