Header Ads


BARAZA LA EID MKOA WA TANGA

Hassan Hashim Tanga.

Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba amelishari Baraza kuu la waislam Tanzania Bakwata mkoa wa Tanga kuwashirikisha vijana wa wasomi ili waweze kutambua wajibu na nafasi yao ndani ya taasisi hiyo katika kupanga mikakati ya maendeleo na kuleta umoja ndani ya dini yao

Rai hiyo ameitoa wakati akihutubia waumini katika baraza la eid mkoa liliofanyika jijini hapa.

Amesema kutowahusisha vijana wasomi katika baraza hilo kunaondoa dhana ya kujenga umoja na mshakamano na kusababisha makundi miongoni mwa Bakwata na waumini wa kiislam.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela amewataka waumini kuendeleza amani na mshikamano na kumuunga mkono rais Magufuli katika juhudi za kupigani raslimali za taifa.


Awali akizungumza baada swala ya Eid mwenyekiti wa kamati ya mwezi mkoa wa Tanga Sheikh Mohamed Yahaya amesema muandamo wa mwezi unakanuni ambazo zinahitaji elimu yakutosha na kuwataka wawaumini  kutoyumbishwa .

………………………..


KATIBU WA BAKWATA  WILAYA TANGA SHEIKH UDAY MBUKUZI AKISOMA RSALA KWA MGENI RASMI

MKUU WA MKOA WA TANGA MARTIN SHIGELA AKIZUNGUMZA KWENYE BARAZA LA EID





WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA JANUARI MAKAMBA AMBAYE ALIKUA MGENI RASMI  KATIKA BARAZA LA EID  AKIZIZTIZA JAMBO


SHEIKHE WA MKOA WA TANGA JUMA LUWUCHU AKIZUNGUMZA



No comments:

Powered by Blogger.