Header Ads


WAMILIKI 18 WA VIWANJA WADAIWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA BILIONI 1.1

 Hassan Hashim Tanga.

Mashauri 18 ya madai ya kodi ya ardhi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 yamewasilishwa katika Baraza  la ardhi na nyumba  wilaya ya Tanga ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuwabana wamiliki wa viwanja wanao kwepa kulipa kodi.

Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa mashuari hayo mwakilishi wa afisa ardhi msaidizi kanda ya kazikazini Thadeus Riziki amesema hatua ya kuwafikisha mahakamani wamiliki wa viwanja  hivyo ni kupata kibali kitakacho wezesha wizara kulipwa makusanyo ya madeni

Amesema baada ya halmashauri kuwapelekea wamiliki hati ya madai na kushindwa kulipa hatua inayofuata ni kuwafikisha mahakamani ili kupata ridhaa ya kisheria ya kukamata mali za wadaiwa.

Kwa upande wake afisa ardhi mteule Halmashauri ya jiji  la Tanga Straton Thobias amesema katika mwaka wa fedha wa 2016/7 halmashauri imeweka lengo la  kukusanya kodi ya ardhi kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.3

Akizungumzia zoezi hilo mwanasheria ofisi ya kamishina wa ardhi  Rosemery Mshana amesema wamiliki wa ardhi wanatakiwa kilipa kodi bila shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa mahakamani  mujibu wa kifungu cha  50  cha sheria ardhi namba nne(4) .
………………………………………
AFISA ARDHI MTEULE HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA STRATON  THOBIAS AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI 
ROSEMARY MSHANA MWANASHERIA OFISI YA KAMISHINA WA ARDHI 




No comments:

Powered by Blogger.