Header Ads


HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA WILAYA YA MUHEZA




AKINAMAMA WAKIWA KATIKA MSARAGAMBO WA KUSAFISHA ENEO LA UJENZI 





Add caption




MKURUGENZI  MTENDAJI WA HALMASHAURI YA MUHEZA LUIZ MLELWA AKIMKARIBISHA MKUU WA WILAYA 


MKUU WA WILAYA YA MUHEZA MWANASHA TUMBO AKIHUTUBIA WANANCHI KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA HOSPITALI


SIWANI WA LUSANGA AKIONGOZA AKINAMAMA KUHAMAISHA UCHANGIAJI WA HOSPITALI 

MWENYEKITI WA CCM WILAYA AKIHAMASISHA WANANCHI 

KATIBU WA CCM WILAYA YA MUHEZA MOHAMED MOYO AKIKABIDHI MCHANGO WA WA CCM  MIFUKO HAMSINI KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI  YA WILAYA

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA AKIZUNGUMZA KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA HOSPITALI YA WIALYA 


 ABDULRAHMAN KITOGO MWAKILISHI WA KAMPUNI YA AGRO TANGA  AMBAYO IMETOA ENEO LA EKARI 100 KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI 



Hassan Hashim Muheza.
Harambee ujenzi wa Hospitali ya wilaya.
 ZAIDI YA MILIONI 30 ZACHENGWA


Mkuu wa wilaya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka wananchi
Wilayani humo kujitolea kwa hali na mali kuchangia ujenzi wa hospitali ya wilaya ili kuimarisha utoaji huduma za afya kwa jamii.

Wito huo ameutoa katika mkutano wa harambee na msaragambo wa kusafisha eneo la ujenzi wa hospital ulioyofanyika katika kijiji cha Lusanga “A” wilayani hapa.

Amesema uamuzi  wa ujenzi wa hospitali hiyo ambao haujatengewa fedha katika bajeti ya mwaka huu umelenga kuboresha  huduma za afya kutokana kuongezeka kwa idadi ya watu na uhaba wa vituo vya afya hali inayosababisha msongamano katika hospitali teule.
    
Akizungumza katika mkutano mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya muheza Bakari Mhando amesema  ujenzi wa hospitali utawapunguzia wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma.

atika harambee hiyo jumla ya ahadi za shilingi milioni 30,138,000 zimetolewa mifuko 987 ya saruji mchanga malori 162 mawe  malori 60 na kokoto malori 71 ambapo mafundi mafundi 40 wamejitolea kujenga chini ya usimamizi wa mhandisi wa wilaya ya muheza.


No comments:

Powered by Blogger.