Header Ads


TRA TANGA YAWAFUNGIA WAFANYABIASHARA WALIOLIMBIKIZA KULIPA KODI


CHUO  KIKU CHA ECKENFORD 

MAAFISA WA TRA WAKIBANDIKA MATANGAZO YA KUFUNGA TANGA HOTEL 

BAADHI YA WAFANYAKAZI WA TANGA HOTEL WAKIWA WAMEPIGWA NA BUTWAA 


MAAFISA WA TRA WAKIFUNGA UTEPE KUASHIRIA KUFUNGWA KWA HOTELI HII


Hassan Hashim Tanga.
Tra yafungia wateja wenye madeni

Mamlaka ya mapato nchini (Tra ) mkoani Tanga imezifungia taasisi na  kampuni za Eckenford  za jijini humo baada ya kushindwa kulipa malimbikizo ya kodi mbalimbali hadi mwaka huu .

Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa Tra mkoa wa Tanga Masawa Masatu amesema mamlaka ya mapato imeamua  kuzifungia kuendesha biashara ikiwa ni hatua ya kwanza ya kuwashinikiza kulipa madeni yao na kwamba endapo wa watashindwa kufanya hivyo hatua inayofuata ni kuuzwa kwa mali zilizozouiwa.

Amesema zoezi la kufungia taasisi na kampunini yanayodaiwa  litakua endelevu na kuwataka wafanya biashara wengine  kujitokeza  ili kuepuka usumbufu.


Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo cha Ekenford Prof John Kiango amesema yatari hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuhakikisha deni hilo linalipwa katika muda uliopangwa.


Kodi inayodaiwa katika taasisi hizo ni ongezeko la thamani (Vat) kodi inayotokana na malipo ya wafanyakazi  (PAE)na kodi ya kuendeleza ufundi stadi (SDL) .

……………………………


   

No comments:

Powered by Blogger.