Header Ads


SERIKALI HAITASITA KUSITISHA MRADI WA MAJI WA SOGEA IWAPO MKANDARASI ATAKWAMISHA MRADI HUO.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI JUMAA AWESO AKISAINI KITABU CHA WAGENI KATIKA MRADI WA MAJI SOGEA MAMLAKA YA MJI MDOGO TUNDUMA
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI JUMAA AWESO AKIMWAGA MCHANGA KWENYE MOJA YA MIRADI YA MAJI ALIYOKUWA AKIKAGUA  KATIKA MAMLAKA YA MJI MDOGO TUNDUMA MKOANI SONGWE WILAYANI MOMBA.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI JUMAA AWESO AKIONGEA NA WANANCHI WA TUNDUMA KUHUSU UTATUZIWA KERO ZA MAJI KATIKA MAMLAKA YA MJI MDOGO TUNDUMA.
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI JUMAA AWESO AMUAGIZA MKANDARASI WA MAJI MBELE YA WANANCHI WA TUNDUMA KUTOKWAMISHA MIRADI YA MAJI ALIYOPEWA KUJENGE


NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI JUMAA AWESO AKICHOTA MCHANGA KATIKA MRADI WA MAJI ULIOPO TUNDUMA WILAYANI MOMBA

Naibu  waziri  wa  maji  JUMAA AWESO ameagiza shs bilioni moja zilizotolewa na Rais JOHN MAGUFULI kwa ajili ya mradi wa maji eneo la SOGEA katika mji mdogo wa TUNDUMA wilaya yaMOMBA mkoani SONGWE zinakamilisha mradi huo. 

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo AWESO amesema mkandarasi aliyepewa kujenga mradi huo kampuni ya Best  one  company   iwapo  atashindwa kukamilisha  mradi  huo  kwa wakati hawatasita  kumchukulia  hatua,

Amesema  mkandarasi huyo akishindwa kukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa serikali haitasita  kumsimamisha  kazi, hali inayochangia kero ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa  eneo la SOGEA

Mkuu  wa  wilaya  ya  MOMBA  JUMA IRANDO ameitaka idara ya maji kutowapa tenda wakandarasi wanaotuhumiwa kukwamisha juhudi za serikali za kukabiliana na tatizo la maji

Imedaiwa  kuwa baadhi ya miradi ya maji wilayani MOMBA inashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na uwezo mdogo wa kitaalamu wa baadhi ya wakandarasi




No comments:

Powered by Blogger.