Header Ads


WAHITIMU WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA.

MAANDANO YA  WANAOHITIMU WA CHUO CHA UFUNDI STADI VETA TANGA




BAADHI YA WANAFUNZI WA CHUO CHA UFUNDI VETA WAKIONYESHA UBUNIFU WA MAVAZI AINA MBALIMBALI




 KAIMU MKUU WA CHUO HAMENYA NTABAYE AKISOMA TAARIFA KWA MGENI RASMI

MGENI RASMI KAIMU DAS SULEIMANI ZUMO AKIHUTUBIA WAHITIMU CHUO CHA UFUNDI VETA TANGA

























RAIS WA CHUO TUMAINI SHAYO AKISOMA RISALA KWA MGENI RASMI


VIJANA  nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na Halimashauri nchi kwa ajili ya kujiajiri na kujiongezea kipato badala ya kusubiri ajira za kuajiriwa .
Rai hiyo imetolewa na kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Suleiman Zumo wakati wa mahafali ya 41 ya chuo cha Ufundi Veta Mkoa wa Tanga
Amesema kuwa serikali  tayari imeshaweka mazingira ya uwezeshaji kiuchumi kwa makundi ya vijana na wanawake hivyo ni jukumu la walengwa kuja na mpango utakaoweza kuwakwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa chuo Hamenya Ntabaye ameiomba serikali kuboresha miundombinu ya kielimu chuoni hapo ikiwemo vifaa vya kisasa ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia.

Ufundi stadi ndio kimbilo  la vijana wengi kwa sasa kutokana na changamoto ya ukosefu wa ajira hivyo uwekezaji wa kimiundombinu katika chuo hicho unahitajika kwa sasa

Jumla ya wahitimu wapato 246 wamefanikiwa kuhitimu mafunzo yao kupitia fani mbalimbali chuoni hapo

MWISHO

No comments:

Powered by Blogger.