Coastal Union yajiimarisha ndani na nje ya uwanja
Hassan Hashim Tanga
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti
wa Timu ya African Sports wana
kimanumanu Hassan Kessy na baadae
kujiuzulu wadhifa huo, ametangaza rasmi
kuachana na timu hiyo yenye maskani yake barabara ya 12 na kuunga mkono Mahasimu wao Jadi timu ya Coastal Union katika jitihada za kunusuru timu hiyo kubaki
katika ligi daraja la kwanza.
Akitangaza uamuzi wa
kujiondoa African sports Kessy amesema
amefikia hatua hiyo kwa hiari yake mwenyewe na kwamba atashirikiana na uongozi
wa Coastal union ili kuhakiksha timu
hiyo inarudi kucheza ligi kuu.
"Nimejiunga na Coastal kwa mapenzi yangu kama nilivyoitwa hapo awali na African Sports na kuisadia hadi kupanda hadi ligi kuu lakini baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti ilitokea kutoelewana na baadhi ya wenzngu nikaamua kujiuzulu lakini leo hii nimeamua kutangaza kuungana na viongozi Coastal union ili kuisadia timu hiyo"
Kwa upande wake mwenyekiti
mstaafu wa Coastal Union Ahmed Aurora amesema wameupokea kwa mikono miwili ujio
wa Kessy na kuahidi kushirikiana naye katika
harakati za kuleta ushindi katika klabu hiyo iliyoshuka daraja msimu uliopita.
Kessy atakumbukwa na
wapenzi na wanachama wa African Sports kwa jitihada zake za kuipandisha timu ya
timu hiyo hadi ligi kuu baada yakushindwa kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka
25.
Mwisho
No comments: