Header Ads


Hapa kazi waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalim akiwasili katika kijiji cha Mgambo wilayani Muheza Kukagua huduma za afya

Hassan Hashim Muheza.
Bilioni 64 kuboreshaji sekta ya Afya.

Serikali imetenga milioni mia tatu (300.mln) kwa kila halmashauri nchini ili kuboresha vituo vya afya  kwa kujenga chumba cha upasuaji wodi ya wazazi  maabara ya damu na  nyumba za watumishi 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake wilayani Muheza.

Amesema uboreshaji wa vituo vya afya utawekewa vigezo na utaratibu maalum kwa kuangalia maeneo ya pembezoni ambayo yamekua na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara.

 "Serikalii imepata Bilioni 64 kutoka Benki ya dunia mkakati uliopo hivi sasa ni kuboresha kituo cha afya kila wilaya  kwa kujenga chumba cha upasuaji, wodi ya wazazi, maabara ya damu na nyumba za watumishi.."  .


Akizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupokea malalamiko ya wananchi waziri Ummy amewataka watumishi kufuata taratibu na maadili ya kazi yao na kumpa siku kumi na nne (14)Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya muheza Luiza Mlelwa kupeleka mganga katika zahanati ya Mgambo ambapo zaidi ya kaya 3000  zinahudumiwa na wauguzi wawili.

Aidha waziri aliwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii CHF ambao utawawezesha kupata huduma katika zahanati, vituo vya afya na hospitali teule wilayani humo. 


katika mkutano huo Waziri Ummy aliahidi kutoa mifuko mia moja ya saruji kusaidia ujenzi wa kituo cha afya cha mgambo kilichopo umbali kilomita 45 kutoka muheza ambapo mbunge wajimbo hilo Balozi Adadi Rajabu aliahidi Mabati hamsini na mifuko mia moja ya saruji.
mwisho .


No comments:

Powered by Blogger.