Header Ads


Jeshi la Polisi mkoani Tanga lafanikiwa kupunguza idadi ya ajali za barabarani mwaka 2016


Na Hassan Hashim Tanga. 
Jeshi la Polisi  mkoani tanga limefanikwa kudhibiti na kupunguza idadi ya matukio ya ajali za barabarani kutoka  109 mwaka 2015 hadi kufikia 91mwaka huu  na hivyo kupunguza ajali za vifo  kutoka 93 hadi 68.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Tanga mrakibu msaidizi Nassoro Sisiwaya katika maadhisho ya wiki ya nenda kwa salama barabarani mkoani Tanga.

Amesema katika ajali hizo kwa mwaka huu watu  80 wamepoteza maisha ukilinganisha na mwaka uliopita ambapo  watu 121 walifarika kwa ajali za barabarani .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amesema ajali za barabarani  zitapungua  endapo wananchi watafuata  taratibu za usalama na maderva  kuzingatia sheria na  mafunzo wanayopata.

Naye Hassan Ramadhani ambaye ni mmoja wa maderva waliotunukiwa  cheti kwa mwaka wa pili mfululiozo kwa kufuata sheria za usalama barabarani  ameliomba jeshi la polisi kuangalia uwezekano wa kutumia kamera zenye uwezo  wa kutambua maderva wanao vunja sheria nyakati za usiku


Kaulimbiu ya maadhisho hayo ni  hatutaki ajali tunataka kuishi salama
………………………………………

No comments:

Powered by Blogger.