Mwakyembe awataka wananchi kutimiza wajibu wao
Hassan Hashim Lushoto.
Waziri wa sheria na mambo
ya Katiba Dk Harrison Mwakyembe ameitaka jamii kutimiza wajibu wao kwa kutoa
taarifa katika ngazi husika ili waweze kupata haki yao badala ya kulalamika
kutotendewa haki na vyombo vya sheria.
Kauli hiyo ameitoa katika
hafla ya kutunuku Astashahada na stashahada kwa wahitimu 343 katika mahafali ya
16 ya chuo cha Mahakam wilayani Lushoto.
Amesema Serikali imeweka
utaratibu mzuri kwa kuunda kamati
za maadili katika ngazi mbalimbali ambazo zinauwezo wa kupokea na
kushuhulikia malalamiko kuanzia mahakama za mwanzo wilaya hadi mahakama kuu.
Aidha waziri Mwakyembe
amesema serikali imeshapeleka bungeni mswaada wa msaada wa kisheria ambao
utawezesha wananchi wasiokua na uwezo kupata huduma hiyo bila malipo.
Naye
Mkuu wa chuo hicho Dkt Paul Kihwelo amesema katika kukabiliana na changamoto ya
udahili wamebuni mifumo mbalimbali ya
kidigital ili kuvutia wanafunzi wengi kujiunga
na chuo hicho.
Kwa
upande wao baadhi ya wahitimu wamesema elimu waliyoipata wataitumia kwenda kukabiliana na changamoto iliyopo
katika jamii husasan akina mama wanaokosa haki zao na watoto wanaoathiriwa na vitendo vya
unyanyasaji na ubakaji.
Mwisho
No comments: