Timu ya mpira wa pete makao makuu ikimenyana na Bandari Mtwara mako makuu walishinda 22-14
HASSANHASHIM TANGA .
MICHEZO .
Mashindano ya michezo ya
timu za Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (Interport Games )yameanza kutimua vumbi katika viwanja
vya Shule ya sekondari Popatlal na Bandari mkoani Tanga.
Katika michezo ya fungua
dimba iliyofanyika asubuhi timu ya mpira wa kikapu ya Tanga imeisambaratisha
makao makuu kwa pointi 77- 42 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa
Bandari ambapo katika mchezo wa soka bandari Dsm imechapa Tanga kwa mabao 3-0.
Kwa upande wamchezo wa
pete makao makuu wameifunga mtwara mabao 22-14 ambapo katika mchezo wa kuvuta
kamba wanawake dar wamewashinda Tanga
kwa 2-0 wakati kwa wanaume Tanga wameibuka naushidi dhidi ya bandari dar
Wakizungumza na channel
ten baadhi ya makocha Fazal Mohamed wa Tanga na Adam Mwaipopo wa Dar es salaam
wametamba kuwa timuzao zimejiandaa vya
kutosha kuibuka na ushindi wa mchezo hiyo .
Mashindano hayo ya siku
nne yanashirikisha michezo ya Soka ,Mpira wa kikapu , Pete, Bao, kuvuta Kamba
na Riadha ambapo yanatarajiwa kufunguliwa na Mkurugenzi wa Bandari Tanzania
mhandisi Deusdedit Kakoko.
………………………
No comments: