Hili ni eneo la kuingiza Magari
Hassan Hashim Tanga.
Kero ya usafiri yapatiwa
ufumbuzi .
Kero ya usafiri kati ya
Tanga na visiwa vya Pemba na unguja inaelekea kupatiwa ufumbuzi wa kudumu baada
ya meli kubwa ya kampuni ya Azam marine kuwasili katika bandari ya Tanga.
Kuwasili kwa meli hiyo kubwa ambayo ina uwezo wa
kubeba abiria 1600 pamoja na magari 50 huenda ikawa ukombozi kwa wananchi
wa maeneo hayo ambao kwa muda mrefu wamekuwa
wakitumia usafiri wa majahazi .
Baadhi ya abiria waliopata
fursa ya kuzungumza na channel ten wameeleza hisia zao kuhusu adha waliyokuwa
wakipata ikiwa ni pamoja na kupoteza ndugu zao kutokana na ajali za majahazi.
Kwa upande wake mkurugenzi
wa ulinzi na usalama ambaye pia ni msajili wa meli kapten Mussa Mandia ametoa wito kwa wamiliki
wa majahazi kuacha kubeba abiria na kuhatarisha maisha ya wananchi .
Akizungumzia ujio wa meli
hiyo katika bandari ya tanga meneja mkuu wa Azam Marine Husein Mohamed Said
amesema wameanza kutoahuduma hiyo baada ya kupokea maombi mbalimbali kutoka kwa wananchi na
serikali.
Januari 10 mwaka huu
jahazi liliokua na shehena ya mizigo na abiria lilizama baada ya kupigwa na tufani ambapo watu 12
walifariki na wengine 27 kujeruhiwa
…………….
No comments: