Kaimu Afisa Forodha kituo cha Horohoro Abraham Maleko (Kushoto) akimweleza Naibu waziri kuhusu tatizo la maji katika kituo hicho
Hassan Hashim Horohoro.
Naibu waziri wa Mambo ya
nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Suzan Kolimba amesema suala la
wakazi wa Mkinga wenye asili ya Kenya ambao wanaoishi nchini kwa muda mrefu
linashughilikwa na wizara ya mambo ya ndani ambayo ndiyo yenye mamlaka ya
kusajili wageni.
Kauli hiyo ameitoa katika mkutano wa hadhara
baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao wakati wa ziara yake mkoani
hapa.
Amesema Serikali hadi sasa
imetambua raia 9083 wenye asili ya makabila ya wakamba waduruma na Wataita
wanaoishi katika wilaya ya Mkinga na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea
kufanyika kabla ya kutolewa uamuzi.
Akitoa taarifa kwa naibu waziri Mkuu wa wilaya ya
Mkinga Yona Maki amesema halmashauri imepima viwanja 1000 vya biashara na
makazi ili kuongeza chachu ya maendeleo katika eneo la Horohoro lakini uwepo wa wahamiaji hao wa muda mrefu ni
chagamoto inayo hitaji ufumbuzi.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri
ametembela na kuzungumza na watumishi wa mpaka wa Hororo nchini Tanzania na Lunga lunga nchini Kenya.
……………………………………
No comments: