Kaimu mkurugenzi wa Nimr Dkt William Kisinza (kushoto) mwenye suti akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya kuhusu eneo kitakapojengwa chuo kikuu cha utafiti wa magonjwa ya binaadam huko Amani wilayani Muheza mkoani Tanga
Hassan Hashim Muheza
NIMR Amani kujengwa chuo kikuu cha utafiti
Waziri wa Afya Ustawi wa
jamii Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu ameitaka taasisi ya utafiti wa magonjwa ya
binadamu (NIMR) kuharakisha uanzishaji wa chuo cha utafiti wa magonjwa ya
binadamu ili kuongeza wataalamu katika
sekta hiyo.
Akizungumza wakati
alipotembelea eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 200 ambalo inakusudiwa kujengwa
chuo kikuu cha afya na utafiti wa magonjwa ya binadamu Waziri Ummy amesema
mpango huo utasaidia kupunguza uhaba wa wataalmu mbalimbali wanaohitajika katika sekta hiyo.
Aidha waziri ummy
amewataka wataalamu wanaofanya utafiti katika taasisi mbalimbali nchini
kufuata utaratibu uliowekwa kutangaza
matokeo yas tafiti zao na kusisitiza kuwa hadi sasa haijathibitika kuwepo kwa
ugonjwa wa ZIKA .
Kwa upande wake Kaimu
mkurugezi Dkt William Kisinza amesema Shirika
la afya duniani WHO limeteua Taasisi ya
utafiti wa magonjwa ya binadamu Nimr Amani kuwa kituo cha kufanya tathmini matumizi
ya viwatilifu katika bara la Afrika.
Naye mbunge wa jimbo la
Muheza Balozi Adadi Rajabu amesema kuanzishwa kwa chuo kikuu cha utafiti katika
eneo la amani kutachochea maendeleo na
uchumi katika wilaya ya muheza.
Mwisho
………………………………..
No comments: