MEYA AKITOA NENO LA SHUKURAN
HASSAN HASHIM TANGA
Shule ya watoto wenye
ulemavu Pongwe yapata msaada wa Gari.
Taasisi ya mfuko wa
maedeleo ya jamii Tanzania (CDTF) imetoa misaada mbalimbali yenye thamani zaidi
ya shilingi milioni 90 kwa shule ya Msingi ya Pongwe ambayo ni malum kwa watoto
wenye ulemavu
Akizungumza katika hafla
ya kukabidhi msaada gari mkurugenzi wa
CDTF Henry Mgingi amesema taasisi hiyo imejitolea baada ya kubaini changamoto
mbalimbali ikiwemo usafiri wa kuwapeleka
hospitali watoto wenye ulemavu katika shule hiyo.
Amesema CDTF baada ya
kupokea mahitaji ya shule hiyo imejitolea kuwalipia bima ya afya watoto wenye
ulemavu wa ngozi na kuanza mradi wa
ujenzi wa bweni katika shule hiyo
Akipokea msaada huo Meya
wa jiji la Tanga Mhina Mustafa Selebos
ameipongeza CDTF kupitia shirika la Emirates kwa msaada huo na kusema
utapunguza tatizo la usafiri kwa wanafunzi hao na kutoa rai kwa watendaji
kwa gari hilo kutumika kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Awali Kaimu mkurugenzi jiji la Tanga Ramadhan Possi
ameishukuru taasisi na kuahidi kuwa
halmashauri itabeba gharama zote za matumizi ya gari hilo
Shule ya msingi Pongwe
inajumla ya wanafunzi 1000 ambapo zaidi ya wanafunzi themanini (80) ni walemavu wenye mahitaji maalum.
………………………………….
No comments: