Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanaasha Tumbo akihutubia wananchi wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji
Na Hassan Hashim Muheza.
Mkuu wa wilaya Muheza
Mhandisi Mwanaasha Tumbo amewataka wananchi waliovamia maeneo ya shamba la LEWA
ambalo limetwaliwa na serikali kuacha kupanda mazao ya kudumu hadi utaratibu wa
kugawanya shamba hilo utakapokamilika .
Kauli hiyoameitoa wakati
akihutubia wananchi katika hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji katika kijiji
cha Kibaoni kata ya Mtindiro wilayani Muheza.
Amesema lengo la serikali
kutwaa shamba hilo ni kuwawezesha wananchi kupata maeneo ya kufanya shughuli za
kilimo na ufugaji na kwamba utaratibu wa matumizi bora ya ardhi utakapokamilika
watapatiwa maeneo bila upendeleo.
Aidha mkuu huyo wa wilaya
amepiga marufuku vitendo vya ukataji
miti na usafirishaji magogo kutoka wilayani humo na kwamba watakaokiuka watakamatwa wao pamoja na magari
yatakayohusika kutaifishwa.
Awali mbunge wa jimbo la Muheza Adadi Rajabu amesema
serikali ipo kwenye mchakato wa kutekeleza mradi mkubwa ambao utaondoa kero ya
maji katika wilaya hiyo.
Jumla ya kaya 2000
zitanufaika na mradi huo ambao ujenzi wake umegharimu milioni 48.6 na
kufadhilwa na kampuni ya Neelkanth .
…………………………………
No comments: