Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akisistiaz jambo
Hassan Hashim Tanga.
Bomba la mafuta
Naibu waziri wa mambo ya
nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Dkt Suzan Kolimba ameitaka halmashauri
ya jiji la Tanga kuwaelimisha wananchi ili waweke mipango itayowasaidia kunufaika
na fursa ya mradi wa bomba la mafuta.
Rai hiyo ameitoa
wakati akizungumza na viongozi wa wilaya
na halmashauri alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa bandari ya kupokelea
mafuta kutoka nchini Uganda katika kijiji cha chongoleani jijni hapa.
Amesema ni muhimu kwa
halmashauri kuweka kipaumbele kwa kufikiria namna kuwanufaisha na mradi wananchi ambao mashamba yao yatachukuliwa
katika utekelezaji wa mradi ili wapate
shughuli mbadala za kuwaingizia kipato.
Awali akitoa taarifa kwa
Naibu waziri Kaimu mkuu wa idara ya mipango miji ardhi na makazi jiji la Tanga
Shabani Mruma amesema Halmashauri imeanza mchakato wa kukusanya taarifa za
utafiti katika maeneo yatakayoathiriwa na mradi wa ujenzi wa Bomba la mafuta
kutoka Uganda ili kurahisisha gharama za fidia wakati wa utekelezaji wa mradi
huo.
Baadhi ya makampuni yameanza
kufanya utafi ili kubaini uwezo wa miamba katika maeneo itakapojengwa bandari
hiyo .
Mwisho.
No comments: