MKUU WA MKOA WA MANYARA JOEL BENDERA (KUSHOTO) NA KATIBU TAWALA WA MKOA HUO ELIAKIM MASWI WAKIFUATILIA KWA MAKINI KIKAO CHA KUJADILI MGOGORO WA MPAKA KATI YA WILAYA ZA KILINDI NA KITETO
Hassan Hashim Tanga
Waziri wa Ardhi nyumba na
maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi
amewaagiza wakuu wa mikoa ya Tanga na Manyara kutoa elimu ya kutosha
kwa wananchi ili kurahisisha zoezi la kuhakiki mpaka kati ya wilaya ya Kiteto
na Kilindi.
Agizo hilo amelitoa katika
mkutano wa Kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka kati ya mikoa ya Tanga na manyara ambao umeshirikisha
wakuu wa mikoa hiyo, makatibu tawala, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri pamoja na maafisa ardhi.
Amesema serikali
imedhamiria kumaliza kabisa mgogoro wa mpaka kati ya wilaya ya Kiteto na
Kilindi na kwamba utoaji elimu utasaidia wananchi kupata uelewa na kutoa ushirikiano
kwa maafisa watakaohusika na zoezi hilo.
Kwa upande wao wakuu wa mikoa ya Tanga na Manyara
wamesema baada ya mkutano huo kitakachofuata ni kufanya uhamasishaji ili
kutekeleza maazimio yaliyokubaliwa.
Mgogoro wa mpaka kati ya
kiteto na kilindi umedumu kwa muda mrefu na kusababisha uvunjifu wa amani
uhasama baina ya wananchi maeneo hayo .
No comments: