Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin shigela akihutubia wananchi katika hafla ya uzinduzi wa kuhakiki wahamiaji walowezi
Na, Hassan Hashim, Mkinga.
Serikali yazindua Usajili
wa wahamiaji walowezi.
Serikali imewaonya
wahamiaji wasiokua na sifa kutojipenyeza katika zoezi la kuhakiki wahamiaji
walowezi na kwamba watakaobainika kuvuruga zoezi hilo watashughulikiwa kwa
mujibu wa sheria za nchi.
Rai hiyo imetolewa na mkuu
wa mkoa wa Tanga Martin Shigella katika hafla ya Kitaifa ya uzinduzi wa zoezi la kuandikisha
wahamiaji walowezi walioishi nchini kwa
muda mrefu iliyofanyika katika kijiji cha Moa mkoani hapa.
Amesema serikali inaendesha
zoezi hilo kwa uwazi na umakini mkubwa na kwamba watakao timiza vigezo
watapatiwa haki bila upendeleo na kupata fursa ya kushiriki katika shughuli za
uzalishaji mali na kuinua uchumi wa taifa
Akizungumza katika
uzinduzi huo naibu kamishina uhamiaji anayesimamia udhibiti wa mipaka Wilson
Bambaganya amesema zoezi la kutafuta ufumbuzi wa suala la wahamiaji walowezi linafanyika nchini kote
kupitia ufadhili wa shirika la IOM .
Kwa upande wao baadhi ya
wananchi wamesema zoezi la kuhakiki wahamiaji walowezi litasaidia kudhibiti
uhalifu katik maeneo ya mipakani.
Wilaya ya mkinga
inakadiriwa kuwa na wakimbizi walowezi 9083
…………………………………………………….
No comments: