Header Ads


Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Muheza Rwebangira Karuwasha abwanga manyanga ahamia CCM

Hassan Hashim.
Mwenyekiti wa CDM MUHEZA ajiuzulu

Siku chache baada ya Uongozi wa Chadema Mkoa wa Tanga kuondolewa  madarakani aliyekua  mwenyekiti  wa chama hicho wilaya ya Muheza  Rwebangira Karuwasha  ametangaza kujiuzulu uanachama kwa madai ya kutoridhishwa na maamuzi yanayotolewa na uongozi wa Taifa.
Akitangaza Uamuzi huo kwenye mkutano wa waandishi wa habari Rwebangira amesema amefikia hatua ya kujiondoa Chadema na kujiunga na CCM ili kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli ambaye ameonyesha nia ya dhati kupambana na ufisadi na kutetea wanyonge.

Amesema kabla ya kufikia uamuzi huo ametafakari kwa kina na kubaini kasoro kadhaa ndani ya Chadema ambapo wanachama hapewi nafasi ya kuziondoa  na kukifanya chama hicho kupoteza mwelekeo kwa kufuata matakwa ya kundi la watu wachache.



Akizungumzia kuondolewa  madarakani kwa  viongozi wa Chadema wilaya na  mkoa Rwebangira  amesema uamuzi wa chama hicho haukuzingatia haki na badala yake unaendeleza chuki na makundi yanayoweza kukibomoa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.


Hivi karibuni Kamati kuu ya Chadema iliwavua madaraka viongozi wa wilaya na mkoa wa Tanga kwa madai ya kushindwa kutekeleza majukumu yao

………………………..

No comments:

Powered by Blogger.