MAREKANI YATISHIA KUIADHIBU KOREA KASKAZINI
Korea Kaskazini imedai
kwamba kombora la masafara marefu ililolifanyia majaribio siku ya Jumapili ni
kombora jipya linaloweza kubeba kichwa cha nyuklia .
Kombora hilo
lililorushwa lilienda anagani urefu wa kilomita 2,000 na kusafiri kilomita 700
kabla ya kuanguka katika bahari Magharibi mwa Japan.
Korea Kaskazini
ilisema siku ya Jumatatu ni jaribio la uwezo wa kombora jipya.
Jeshi la Korea Kusini
limesema kuwa haliweza kuthibitisha madai hayo ya Korea Kaskazini.
Lakini limesema kuwa
kombora hilo lilionekana kuweza kuruka angani, hatua ambayo ni muhimu katika
utengenezaji wa makombora ya masafa marefu kulingana na kituo cha habari cha
Yonhap.
Majaribio ya mara kwa
mara ya makobora ya masafa marefu yanayofanywa na taifa hilo yanakiuka vikwazo
vya Umoja wa Mataifa na yamesababisha wasiwasi miongoni mwa jamii ya kimataifa
pamoja na Marekani.
Marekani na Japan
zimetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa siku ya Jumanne.
Shirika la habari la
Korea Kaskazini KCNA limesema Jumatatu kwamba jaribio la kombora jipya la
masafa marefu la Hwasong 12 lilifanyika kama ilivyopangwa.
Limesema kuwa jaribio
hilo lililenga kuonyesha kwamba kombora hilo jipya lina uwezo wa kubeba kichwa
cha Nyuklia.
Chanzo bbc swahili
No comments: