NA Hassan Hashim, Tanga.
King Majuto asikitishwa na
uzushi wa mitandao ya kijamii
Msanii gwiji wa maigizo ya
vichekesho nchini Amri Athuman (King Majuto) ametoa rai kwa watanzania kuwa
makini katika matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo kwa kiasi kikubwa imekua
ikitumika vibaya na kuleta madhara kwa jamii.
Kauli hiyo ameitoa katika
mahojiano maalum yaliyofanyika nyumbani kwake Donge kufuatia uvumi uliozagaa
nchini kupitia mitandao ya kijamii kwamba amefariki dunia.
Amesema kitendo cha kusambaza
habari za uzushi wa kumhusisha yeye kwamba amefariki zimeleta mshituko mkubwa
na usumbufu kwa familia yake pamoja na marafiki na kuiomba serikali kuwadhibiti
wanatumia vibaya mitandao ya kijamii.
Majuto amesema kitendo
kuzushiwa kifo kimejirudia zaidi ya mara tano sasa hali inayoonesha kwamba
huenda kuna watu ambao wanafanya hivyo kwa malengo maalum wanayoyajua wenyewe
na kuongeza kuwa anawasiliana na mwanasheria wake ili kuchukua hatua stahiki.
Akizungumzia hali yake
kiafya Majuto amesema julai 15 mwaka huu alilazwa katika kituo binafis cha
Tanga Health centre na kufanyiwa upasuaji
mdogo wa hernia na kuruhusiwa julai 18 ambapo kwa sasa anaendelea na mazoezi madogo nyumbani
kwake.
MWISHO
|
No comments: