Header Ads


HAFLA YA KUKABIDHI MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAJI SAFI KUTOKA PONGWE HADI MUHEZA



AFISA UHUSIANO MAMLAKA YA MAJI TANGA UWASA DORA KILLO AKIKARIBISHA WAGENI 

MKURUGENZI MTENDAJI WA TANGA UWASA MHANDISI JOSHUA MGEYEKWA AKITOA MAELEZO KUHUSU UJENZI WA MRADI HUO  

MSIMAMIZI WAUJENZI WA MRADI MHANDISI FARES ARAM 


MGENI RASMI MBUNGE WA JIMBO LA MUHEZA BALOZI ADADI RAJABU 

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILYA YA MUHEZA LUIZA MLELWA 

SHEHENA YA MABOMBA YATAKAYOTANDAZWA KATIKA MRADI HUO 



MKANDARASI AKITOA MAELEZO KWA VIONGOZI WA HALMASHAURI NA TANGA UWASA




 Hassan Hashim Muheza.
Utekelezaji wa ahadi ya Rais.

Kampuni ya Kobarg imekabidhiwa rasmi ujenzi wa mradi wa majisafi  kutoka Pongwe wilayani tanga hadi  muheza ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya rais aliyoitoa katika kijiji cha mkanyageni wakati wa ziara yake mkoani tanga.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi ujenzi wa mradi huo unaosimamiwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Tanga  mbunge wa wilaya ya muheza Balozi Adadi Rajab amesema mradi huo wenye urefu wa kilomita 19 ni moja ya juhudi za serikali kumaliza tatizo la maji wilayani humo.

Amesema mradi huo ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miezi tisa ni moja kati ya miradi kadhaa ambayo serikali imeahidi kuitekeleza.
         
Awali  mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi jiji la tanga mhandisi Joshua Mgeyekwa amewahakikishi wakazi wa jiji hilo kwamba hatua ya kupeleka maji wilayani muheza haitaathiri utoaji wa huduma za Mamlaka .

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Muheza Luiza Mlelwa amesema katika kukabiliana na tatizo la maji halmashauri imetenga kiasi cha shilingi i 50 kwa ajili ya kuchimba visima mia moja katika vijiji mbalimbali.

Agost 5 mwaka huu rais John Magufuli akihutubia wananchi katika kijiji cha mkanyageni aliahidi kushughulikia  kero yamaji  wilayani  muheza.

……………………………………..





No comments:

Powered by Blogger.