Header Ads


ZOEZI LA UHAKIKI WA MIFUGO LAPATA MUITIKIO MKUBWA WILAYA YA HANDENI



Add caption
 Hassan Hashim Handeni.

Wafugaji wilayani Handeni mkoani Tanga wametakiwa kuitikia kwa vitendo agizo la serikali kwa kufikisha mifugo yao katika maeneo husika ili ihakikiwe na kuwekewa alama za utambuzi

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Handen Godwin Gondwe katika hafla ya uzinduzi wa upigaji chapa mifugo  iliyofanyika katika kijiji cha Sua wilayani humo.

Amesema lengo la serikali la kuweka alama za mifugo ni kuwezesha kutambua mifugo iliyopo katika maeneo mbalimbali na kudhibiti uingizaji wa mifugo kiholela kutoka maeneo mengine ambayo imekuwa chanzo cha migogoro  kati ya wakulima na wafugaji .

Kwa upande wao baadhi ya wafugaji wamepongeza zoezi hilo na kuiomba serikali kuharakisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ambao utaanisha maeneo ya malisho ili kuondoa migogogo.

Zaidi ya ng’ombe 1,31,000 Wilaya ya Handeni  wanatarajiwa kupigwa chapa ikiwa ni kutekeleza agizo la serikali la kuhakiki na kutambua mifugo yote iliyopo nchini.

…………………………….

No comments:

Powered by Blogger.