Header Ads


TAASISI ZA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI ZATAKIWA KUWEKA MKAKATI ILI KUFIKIA MALENGO

 WAZIRI WA MAJI ISSACK KAMWELE  AKIHUTUBIA VIONGOZI WA TAASISI ZA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI.


WAZIRI WA MAJI ISSACK KAMWELE   AKIKAGUA MITAMBO YA KUTIBU MAJI TANGA UWASA.
WAZIRI WA MAJI ISSACK KAMWELE AKITEMBELEA KUKAGUA VYANZO VYA MAJI TANGA UWASA
 



























 
Hassan Hashim  Tanga .

Taasisi na Mamlaka za maji  nchini zimetakiwa kuweka mkakati utakaofanikisha kufikia malengo ya serkali upatikanaji wa  huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 75 % ifikapo juni mwaka 2018.

Agizo hilo limetolewa na waziri wa maji mhandisi Issack  Kamwele wakati akifungua mkutano wa mwaka wa mamlaka za maji nchini unaofanyika jijini hapa.

Amesema  uzoefu uliopatkana katika mamlaka za maji mijini kuongeza upatikanaji wa huduma ufikishwe katika ngazi za halmashuari ili kufikia malengo la serikali ya kuboresha huduma za maji kwawananchi wote .

Amesema tangu kuanzishwa kwa program ya maendelo ya maji serikali imelenga kuanzisha  vituo vya  kutolea maji 117,000 lakini kutokana na uharibifu wa mazingir asilimia 35 havitoi maji .
 
Awali akimkaribisha waziri  mwenyekiti ATAWAS  Mkama Bwire amesema
Changamoto iliyopo kwa hivi sasa niupatikanaji wa rasilimali ya uendelezaji wa miradi ya utoaji wa  huduma za maji


Mkutano huo unashirikisha wadau wa sekta ya maji zikiwemo mamlaka vyuo watafiti na watoji wa huduma mbalimbali.

No comments:

Powered by Blogger.