KAMANDA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI NCHINI KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI FOTUNATUS MUSILMU AMEONGOZA UKAGUZI WA MAGARI KWA MIKOA MITATU YA TANGA, PWANI NA KILIMANJARO
KAMANDA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI NCHINI AKIWA NAMWENYEKITI WA BARAZA WAKITOA ELIMU KATIKA MOJA YA MABASI WAKITOA ELIMU KWA ABIRIA |
ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAKIWA KATIKA ZOEZI HILO KATIKA ENEO LA SEGERA MKOANI TANGA |
ASKARI WAKIKAGUA MAGARI |
ASKARI WA USALAMA BARABARANI AKIWA KAZINI |
MOJA YA MAGARI YALIYOKAMATWA KWA MAKOSA MBALIMBALI |
KAMANDA FOTUNATUS AKITOA ELIMU NDANI YA BASI JUMLA YA MAGARI 464 YAMEKAGULIWA KATIKA ZOEZI HILO
Askari akikagua gari katika eneo a Segera mkoani Tanga wakati wa operesheni maalum ya kudhibiti ajali |
Hassan Hashim Tanga
Jeshi la polisi nchini kikosi cha usalama barabarani kimeanzisha operesheni maalumu ya pamoja ya kukagua magari barabarani ili kudhibiti ajali zinazotokea kipindi cha mwisho wa mwaka.
……..
Akizungumza wakati wa operesheni hiyo iliyoshirikisha mikoa ya Tanga Kilimanjaro na Pwani kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Fotunatusi Musilimu amesema zoezi hilo linaendelea nchini kote kwa kushikisha mikoa iliyopo jirani.
Amewataka madereva kufuata sheria za usalama baarabarani na abiria kutoa taarifa pindi wanapoona dereva anaendesha kwa mwendo kasi.
Kwa upande wake afisa mnadhimu wa kikosi hicho kanda ya kaskazini Theopista Mallya amewataka askari wa usalama barabrani kutenda haki wakati wa zoezi hilo ili kuondoa malalamiko.
Katika kipndi cha disemba 29 hadi 31 2017 Jumla ya ajali saba zilitokea na kusababisha vifo vya watu nane na majeruhi wa tano kwa nchi nzima ambapo magari 464 yalikaguliwa na makosa 154 yamebainika.
No comments: