Meya wa jiji la Tanga Mhina Mustafa akitangaza kuwachaukulia hatua watumishi waliokiuka maadili
Hassan HashimTanga.
12 watumbuliwa halmashauri
ya jiji.
Baraza la madiwani katika
halmashauri ya jijila Tanga limewaadhibu Watumishi kumi na mbili baada ya kubainika
kutenda makosa mbalimbali ya kinidhamu kinyume na kanuni za utumishiwa umma.
Akitangaza uamuzi huo Mstahiki
Meya wa jiji la Tanga Mohamed Mustafa
Selebos amesema baada ya kupitia na kujadili tuhuma zilizowasilishwa dhidi ya
watumishi baraza limeridhika na kuchukua
hatua mbalimbli ikiwemo kuwafukuza kazi kuwavua madaraka kuwakata mishahara na
kuwapa barua za onyo kulingana na makosa
husika.
Selebos amebainisha kuwa katika
uamuzi huo Baraza limezingatia haki na sheria na kutambua kwamba kazi inagusa uhai
wa mtumishi.
Kwa upande wake mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya jiji Daudi Mayeji amewataka watumishi kufanya kazi
zao kwa kufuata maadili na kutimiza wajibu bila kuwaonea wananchi wanao
watumikia
Mayeji amewataka wananchi kuacha
tabia ya kutumia mawkala wanapohitaji huduma badala yake watumie ofisi za halmashauri na kupata stakabadhi kwa
malipo wanayofanya
………………………….
No comments: