PICHA MBALIMBALI MATUKIO YA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA WADAU WA VYAMA VYA USHIRIKA
Hassan Hashim Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga
Martin Shigela amevitaka vyama vya ushirika mkoani humo kuunda muungano wa Ushirika ambao utakua na nguvu moja katika kuratibu na kusimamia maamuzi ili kuharakisha maendeleo ya vyama
vya ushirika.
Agizo hilo amelitoa wakati
akifungua mafunzo ya siku moja ya kuhuisha kamati za ushirika mkoani hapa.
Amesema kuundwa kwa muungano
wa umoja wa vyama vya ushirika kutasaidia kuunganisha nguvu nakutumia fursa
walizonazo ili kushughulikia kwa urahisi
changamoto zinazowakabili katika sekta hiyo
Akizungumzia mafunzo hayo Mratibu
na mkufunzi wa chuo cha ushirika tawi la
Tanga Abel Ngoi amesema lengo la mafunzo hayo
ni kuhuisha kamati za ushirika na kuwashirikisha wadau ili waweze
kukabiliana na changamoto zilizopo katika vyama vya ushirika mkoani hapa.
Mafunzo hayo ya siku moja yameshirikisha maafisa ushirika kutoka wilaya zote za za
mkoa wa Tanga pamoja na wadau wa vyama mbalimbali vya ushirika.
………………………….
MKUU WA MKOA WA TANGA MARTIN SHIGELA AKIZUNGUMZA WAKATI WA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA MAAFISA USHIRIKA WILAYA NA WADAU |
BAADHI YA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA KUHUISHA KAMATI ZA USHIRIKA |
WASHIRIKI WA MAFUNZO WAKISIKILIZA MADA |
MRAJISI WA VYAMA VYA USHIRIKA JACKLINE SENGHE AKIMKARIBISHA MKUU WA MKOA KATIKA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA KUHUISHA KAMATI ZA USHIRIKA |
ABEL NGOI MKUFUNZI WA MAFUNZO |
BAADHI YA WASHIRIKI WAKIBADILISHANA MAWAZO NA MKUU WA MKOA |
BAADHI YA WASHIRIKI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA |
No comments: