Na Hassan Hashim. Tanga,
Wataalamu wa ardhi katika
halmashauri ya jiji la tanga wametakiwa kufanya kazi kwa weledi katika upimaji
wa viwanja ili kuondoa migogoro ya mara kwa mara kati ya wananchi na halmashauri.
Kauli hiyo imetolewa na
baadhi ya madiwani wakati wakichangia hoja katika kikao cha baraza
kilichofanyika jijini hapa
Wamesema malalamiko
na migogoro mingi ya ardhi iliyopo hivi
sasa inaweza kuepukika endapo wataalamu watazingatia maadili ya kazi yao wakati
wa kuanisha michoro na upimaji wa viwanja.
Akizungumza katika kikao
hicho mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Tanga Daud Mayeji amesema baadhi ya wananchi wamekua chanzo cha migogoro kwa kubadili matumizi ya maeneo
waliyomilikishwa na kujenga bila kufuata
taratibu na sheria za mipango miji.
Katika kikao hicho baraza
la madiwani lilipitisha azimio la kuhuishwa kwa michoro iliyopo hivi sasa ili
iendane na mahitaji ya sheria za mipango miji.
……………………………………
|
No comments: