BARAZA LA EID MKOA WA TANGA
Hassan Hashim Tanga.
Waziri wa nchi ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira January Makamba amelishari Baraza kuu la waislam
Tanzania Bakwata mkoa wa Tanga kuwashirikisha vijana wa wasomi ili waweze kutambua
wajibu na nafasi yao ndani ya taasisi hiyo katika kupanga mikakati ya maendeleo
na kuleta umoja ndani ya dini yao
Rai hiyo ameitoa wakati
akihutubia waumini katika baraza la eid mkoa liliofanyika jijini hapa.
Amesema kutowahusisha
vijana wasomi katika baraza hilo kunaondoa dhana ya kujenga umoja na mshakamano
na kusababisha makundi miongoni mwa Bakwata na waumini wa kiislam.
Kwa upande wake mkuu wa
mkoa wa Tanga Martin Shigela amewataka waumini kuendeleza amani na mshikamano
na kumuunga mkono rais Magufuli katika juhudi za kupigani raslimali za taifa.
Awali akizungumza baada
swala ya Eid mwenyekiti wa kamati ya mwezi mkoa wa Tanga Sheikh Mohamed Yahaya
amesema muandamo wa mwezi unakanuni ambazo zinahitaji elimu yakutosha na
kuwataka wawaumini kutoyumbishwa .
………………………..
MKUU WA MKOA WA TANGA MARTIN SHIGELA AKIZUNGUMZA KWENYE BARAZA LA EID |
WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA JANUARI MAKAMBA AMBAYE ALIKUA MGENI RASMI KATIKA BARAZA LA EID AKIZIZTIZA JAMBO |
SHEIKHE WA MKOA WA TANGA JUMA LUWUCHU AKIZUNGUMZA |
No comments: