Waziri wa Mifugo na uvuvi Luhaga Mpina Akiangalia taarifa ya kampuni ya stage farm ambayo ni mwekezaji katika vitalu vya ranchi hiyo
Hassan Hashim Handeni.
Waziri wa mifugo na uvuvi
Luhaga Mpina ameagiza kuvunjwa kwa mkataba kati ya ranchi ya Mzeri na Kampuni
ya Overland ambao ilianzisha kampuni ya
OVENCO kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza na kuitaka Narco kutengeneza mkataba
mpya utakaozingatia maslahi ya taifa.
Agizo hilo amelitoa wakati
wa ziara yake katika ranchi Mzeri iliyopo wilayani Handeni ambapo baada ya
kupokea taarifa amebaini kutokamilika kwa uundwaji wa bodi kampuni OVENCO na
kuiacha kampuni ya overland yenye 70% ya hisa kufanya shughuli zake bila usimamizi
wa pamoja.
Amesema Mkataba uliopo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka
miwili uvunjwe ifikapo disemba 31 mwaka huu na kutengeneza mpya ambao utaainisha
thamani ya uwekezaji na ukubwa wa eneo
kulingana na mahitaji ya mwekezaji badala ya kuhodhi ardhi kubwa bila ya kuendelezwa.
..
Aidha Waziri Mpina amesema
pamoja na kasoro zilizopo kwenye mkataba wa uanzishwaji wa Ovenco ameridhishwa
na juhudi za mwekezaji katika kuinua
sekta ya mifugo na kwamba wakati mkataba mpya ukiandaliwa maslahi ya mwekezaji huyo
yatalindwa.
Akizungumzia hatua hiyo ya
waziri meneja uzalishaji uendeshaji ranchi za taifa Bwire Kafumu amesema Narco itafanya uhakiki wa thamani
halisi wa mali zilizopo na kuishauri serikali.
Kwa upande wake mkurugenzi
wa kampuni ya overland Feisal Edha amesema ameridhishwa na hatua ya waziri
ambayo itatoa fursa na haki kwa pande zote
……………………….
|
No comments: