Hassan Hashim Tanga
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka vijana wanaopata mafunzo ya ujasiriamali kupitia taasisi mbalimbali wilayani humo kutumia fursa hiyo kwa kujiletea maendeleo yao binafsi na kuinua uchumi waTaifa.
Rai hiyo ameitoa katika hafla ya kukabidhi vifaa kwa vijana waliopata mafunzo ya ujasiriamali kupitia taasisi BRAC jijini hapa.
Amesema juhudi zinazofanywa na taasisi binafsi kuwawezesha vijana kielimu na hatimaye kuwapatia vifaa hazibudi kuungwa mkono na serikali lakini jukumu kubwa lipo kwa wanufaika kuendeleza miradi hiyo.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi mkufunzi wa mafunzo wa taasisi ya fedha na mikopo ya Brac Manoah William amesema mbali ya kutoa mafunzo na vifaa kwa vijana shirika hilo linaingia mkataba na wahitimu kusaidia vijana wengine wanne kwa mwaka.
Jumla ya wahitimu 74 wa mafunzo hayo wamekabidhiwa vyerahani na mashine za kutengeneza nywele.
|
MKUU WA WILAYA YA TANGA THOBIAS MWILAPWA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUKABIDHI VIFAA |
|
MKUU WA WILAYA YA TANGA THOBIAS MWILAPWA AKIMKABIDHI CHEREHANI MMOJA WA WASHIRIKI WA MAFUNZO( KUSHOTO MWENYE KOTI) NI FIELD TRAINER. MINOLA WILLIAM |
|
BAADHI YA VIJANA WALIONUFAIKA NA MPANGO WA MAFUNZO NA KUPATIWA VITENDEA KAZI |
|
MASHINE ZA KUSHONEA AMBAZO BRAC IMEZIGAWA KWA WAJASIRIAMALI |
|
MANOLAH WILLIAM FIELD TRINER BRAC |
No comments: