IGP SIMON SIRRO ALIPOTEMBELEA TANGA PRESS CLUB
MWENYEKITI TANGA PRESS AKIMKARIBISHA MKUU WA JESHI LA POLISI WAKATI ALIPOTEMBELEA TPC |
MWENYEKITI TANGA PRESS HASSAN HASHIM AKITOA UTAMBULISHO |
MKUU WA JESHI LA POILISI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAANDISHI WA HABARI TANGA |
Hassan Hashim Tanga.
Mkuu wa jeshi la Polisi
nchini INSP Jen Simon Siro amewataka waandishi wa habari kutanguliza uzalendo
kwa kuandika taarifa zinazochochea
maendeleo na kuondoa migogoro kwa wananchi
Kauli hiyo ameitoa katika mkutano na vyombo vya habari
uliofanyika katika ukumbi wa Tanga press club.
Amesema vyombo vya habari
vinawajibu mkubwa wa kuibua fursa za kiuchumi badala ya kuandika habri za
uchochezi
Akizungumzia ziara yake
mkoani Tanga IGP Siro amesema imelenga kumbusha wajibu wa askari katika utendaji kazi na kujiepuka vitendo vinavyochafua sifa ya
jeshi hilo.
Kuhusu masuala ya usalama
mkuu huyo wa jeshi la polisi amesema kwa kushirikiana na vyombo vingine vya
usalama wataimarisha ulinzi katika mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka
Uganda hadi Tanga.
No comments: