NAIBU WAZIRI MALI ASILI NA UTALII RAMO MAKANI AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE WALIPOTEMBALEA MAPANGO YA AMBONI.
Na Hassan Hashim Tanga.
Serikali imetakiwa kuweka
mkakati wa kuimarisha vivutio vya utalii
vya asili ili kuviongezea thamani na kuvutia watalii wengi zaidi.
Rai hiyo imetolewa na
baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi , mali asili na utalii
mara baada ya kutembelea mapango ya Amboni mkoani tanga.
Wamesema Tanzania ni moja
ya nchi ambazo zina vivutio vingi vya malikale lakini imeshindwa kuvitumia
ipasavyo na kulongeza mapato kupitia sekta ya utalii
Akizungumzia mkakati wa
serikali kuhusu uboreshaji wa vivutio vya asili Naibu waziri mali asili na utalii mhandisi Ramo Makani
amesema mwelekeo uliopo hivi sasa ni kuongeza nguvu ya uwekezaji kwa kutangaza vivutio vya mali kale ili
kushawishi watalii wengi kutembelea.
Kwa upande wake kaimu
mkurugenzi idara ya mambo ya kale Digna Tilya amesema wizara malia asili kwa
kushirikiana na wizara ya madini watahakiki mipaka ya maeneo ya mapango ya
amboni ili kukabilaina uharibifu ulipuaji myamba kwa ajili ya kokoto na mawe
……………………………
|
No comments: