Hassan Hashim Tanga.
Wafanyakazi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira jijini Tanga (Tanga uwasa) wamehitimisha maadhimisho wiki ya maji
mwaka huu kwa kujitolea kuchagia damu
salama kwa ajili ya wagonjwa wenye uhitaji wanaolazwa katika hosptali ya rufaa
ya mkoa Bombo.
Akizungumza wakati
wa zoezi hilo Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo Mhandisi Phares
Aram amesema katika maadhimisho hayo mbali ya kutoa elimu kwa kwa wateja
wafanyakazi wameamua kujitolea kuchangia damu salama.
Kwa upande wake mtalamu wa kitengo cha maabara
hospitali ya rufaa ya mkoa Bombo Musara
Abubakar amesema zoezi la hilo la uchangiaji damu salama litaiongezea benki ya
Damu uwezo kutoa huduma bora kwa
wagonjwa wenye uhitaji.
Zaidi ya 90 za damu zimekusnywa katika zoezi hilo lililo shirikisha wafanyakazi wa mamalaka ya maji na wadau.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya maji mwaka huu hifadhi vyanzo vya maji na mifumo ikolojia kwa
maendeleo ya jamii.
………………
|
No comments: