MKUU WA WILAYA YA TANGA THOBIAS MWILAPWA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOSHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI
Hassan Hashim Tanga.
Mkuu wa wilaya ya Tanga
Thobias Mwilapwa ameziagiza kamati za ulinzi za mitaa na kata kuwafichua
wanaojihusisha na uuzaji usambaza na utumiaji wa dawa za kulevya ili waweze
kuchukuliwa hatua na kukomesha tatizo hilo.
Agizo hilo amelitoa wakati
wa matembezi ya hisani ya kuchangia uanzishwaji wa kituo cha kuhudumia
waathirika wa dawa za kulevya (Sober
house) kwa wanawake yaliyoratibiwa na
kituo cha Gift of hope cha jijini hapa.
Amesema utumiaji wa dawa
za kulevya umeathiri vijana wengi ambao ni nguvu kazi na kwamba juhudi za
kupambana na tatizo hilo liwe ni ajenda ya kudumu kuanzia ngazi za familia na mitaa kwa jamii kutoa
ushirikiano ili kubaini wahusika.
Kwa upande wake afisa
maendeleo ya jamii jij la Tanga Mwantumu Dossi amesema halmashauri imeweka
mkakati wa kutoa elimu kwa vijana ili waweze kutambua madhara ya matumizi ya
dawa za kulevya.
Katika matembezi hayo zaidi ya shilingi
milioni nne zimepatikana ikiwa ni fedha taslimu vifaa na ahadi.
……………………………….
No comments: