MKUU WA WILAYA AKISISTIZA JAMBO WAKATI WA UZINDUZI WA MNADA WA KOROSHO KATIKA KIJIJI CHA KIBAFUTA ZAIDI YA TANI 189 ZILIUZWA KATIKA MNADA HUO
Hassan Hashim Tanga
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias
Mwilapwa amewataka wakulima wa korosho mkoani humo kutokubali
kurubuniwa kwa kuuza mazao yao kwa walanguzi na badala yake kupeleka
katika vyama vya ushirika ili waweze kunufaika na jasho lao
Agizo jhilo amelitoa wakati wa mnada
wa korosho uliofanyika katika kijiji cha kibafuta mkoani hapa ambapo zaidi ya
tani 189 ziliuzwa kupitia vyama viwili vya ushirika.
Amesema serikali imeanzisha utaratibu
huo ili kumnufaisha mkulima na kuepuka walanguzi wanao tumia vipimo ambayo sio
shaihi
Akizungumza katika mnada huo mrajisi
wa vyama vya ushirika mkoa wa Tanga Jackline Senzige amesema katika kipindi cha
wiki mbili Bei ya korosho imepanada kutoka shilingi 2650 kwa kilo hadi shilingi
3500 kwa korosho ya daraja la kwanza
Kwa upande wao baadhi ya wakulima
wamesema wameupongeza utaratibu huo na kusema kuwa ndio njia pekee ya
kuwakomboa wakulima ambao kwa muda mrefu amekua wakinyonywa na walanguzi
Katika mnada huo kampuni B
thousand ltd imeshinda tenda ya kununua korosho ya daraja la kwanza
ambapo kampuni Mahenge commodity imeshinda kwa korosho ya daraja la pili.
……………………..
No comments: