WAMILIKI 18 WA VIWANJA WADAIWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA BILIONI 1.1
Hassan Hashim Tanga.
Mashauri 18 ya madai ya
kodi ya ardhi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 yamewasilishwa katika
Baraza la ardhi na nyumba wilaya ya Tanga ikiwa ni mkakati wa Serikali
wa kuwabana wamiliki wa viwanja wanao kwepa kulipa kodi.
Akizungumza mara baada ya
kuwasilishwa kwa mashuari hayo mwakilishi wa afisa ardhi msaidizi kanda ya
kazikazini Thadeus Riziki amesema hatua ya kuwafikisha mahakamani wamiliki wa
viwanja hivyo ni kupata kibali kitakacho
wezesha wizara kulipwa makusanyo ya madeni
Amesema baada ya
halmashauri kuwapelekea wamiliki hati ya madai na kushindwa kulipa hatua
inayofuata ni kuwafikisha mahakamani ili kupata ridhaa ya kisheria ya kukamata
mali za wadaiwa.
Kwa upande wake afisa
ardhi mteule Halmashauri ya jiji la
Tanga Straton Thobias amesema katika mwaka wa fedha wa 2016/7 halmashauri
imeweka lengo la kukusanya kodi ya ardhi
kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa kukusanya shilingi
bilioni 2.3
Akizungumzia zoezi hilo
mwanasheria ofisi ya kamishina wa ardhi
Rosemery Mshana amesema wamiliki wa ardhi wanatakiwa kilipa kodi bila
shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa mahakamani mujibu wa kifungu cha 50 cha
sheria ardhi namba nne(4) .
………………………………………
AFISA ARDHI MTEULE HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA STRATON THOBIAS AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI |
ROSEMARY MSHANA MWANASHERIA OFISI YA KAMISHINA WA ARDHI |
No comments: