NCHI ZA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA (SADC) KUFANYA ZOEZI LA PAMOJA LA KIJESHI TANGA
Hassan Hashim Tanga
Nchi wanachama wa Jumuiya
ya maendeleo kusini mwa afrika SADC zitaendesha zoezi la pamoja la kijeshi kwa
ajili ya kujiandaa na kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhalifu unaoweza
kutokea ndani ya nchi hizo.
Akizungumza katika mkutano
na waandishi wa habari kiongozi wa zoezi
hilo Meja jen Harison Masebo amesema nchi ya Tanzania imekuwa mwenyeji katika
kutekeleza zoezi hilo la kijeshi linafanyika kila mwaka ambalo limepewa jina la
operesheni Matumbawe
Amesema miongoni mwa mambo
yatakayofanyika ni kuwapa askari mbinu za kiulinzi pamoja za kukabiliana na
makundi ya kihalifu
Kwa upande wake Mkuu wa
mkoa wa Tanga MARTIN SHIGELA amewataka wananchi kuwa na utulivu wakati wa zoezi
hilo na kuondoa hofu pindi watakapo waona askari wa kigeni mitaani .
Zoezi hilo linashirikisha
nchi za Tanzania, Zambia, Malawi, Zimbawe,Afrika kusini,Lesotho na Botswana
……………………
MKUU WA "OPARESHENI MATUMBAWE" MEJ..JEN HARRISON MASEBO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KULIA NI MKUU WA MKOA WA TANGA MARTIN SHIGELA |
BAADHI YA WAPIGANAJI KUTOKA NCHI ZA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA SADC WAKIWA KATIKA MKUTANO NA VYOMBO VYA HABARI MKOANI TANGA |
MEJ. JEN. HARRISON MASEBO AKITOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JIJINI TANGA |
Add caption |
No comments: