MKUTANO WA KUELIMISHA WADAU WA SEKTA YA UCHUKUZI KUHUSU MPANGO WA TAIFA WA UTAFUTAJI NA UOKOAJI INAPOTOKEA AJALI KWA NJIA YA ANGA NA MAJINI.
BAADHI YA WASHIRIKI WAKIANGALIA FILAMU INAYOHUSU UTAFUTAJI NA UOKOAJI WAKATI WA AJALI ZA ANGANI NA MAJINI |
MKUU WA WILAYA YA TANGA THOBIAS MWILAPWA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO |
KAIMU MKURUGENZI USALAMA NA MAZINGIRA WIZARA YA UJENZI MAWALIANO NA UCHUKUZI STELA KATONDO AKITOA MWONGOZO KUHUSU MPANGO HUO |
MKUU WAMKOA WA TANGA MARTIN SHIGELA AKIFUNGUA MKUTANO WA WADAU WASEKTA YA UCHUKUZI KUHUSU MPANGO WA TAIFA WA UTAFUTAJI NA UOKOAJI |
WASHIRIKI WA MKUTANO HUO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA |
Hassan Hashim Tanga.
Wadau wa usafiri wa anga na majini wametakiwa kuandaa mapendekezo ya mpango utakaobainsha mamlaka itakayohusika kusimamia uokoaji wakati wa majanga katika sekta hiyo ajali ili kuongeza ufanisi.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela wakti akifungua mkutano wa kuelimisha wadau sekta ya uchukuzi kuhusu mpango wa Taifa wa utafutaji na uokoaji inapotokea ajali za anga na njia za majini.
Amesema kutokuwepo kwa chombo mahususi cha kinachosimamia uokoaji wakati wa ajali za aina hiyo kunachanaganya watendaji na kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amewataka wataalamu wanaohusika kuhakikisha kila chambo kinachofanya safari husuasn majini kimefanyiwa ukaguzi wa kutosha ili kuepusha ajali.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usafirishaji Zanzibar Abdalah Hussein Kombo amesema serikali ya mapinduzi imweka mkakati wa kusimamia Bandari bubu ili kupunguza uwezekano wa kutumika kwa vyombo visivyokuwa na usajili.
Awali Kaimu mkurugenzi usalama na mazingira wizara ya ujenzi mawasiliano na uchukuzi Stela Katondo amesema lengo la mkutano huo ni kupata maoni ya wadau ili kutengeneza sheria itakayowezesha kushirikiana katika utafutaji na uokoaji kwa njia za anga na majini.
…………………………..
No comments: