HAFLA YA KUKABIDHI MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAJI SAFI KUTOKA PONGWE HADI MUHEZA
AFISA UHUSIANO MAMLAKA YA MAJI TANGA UWASA DORA KILLO AKIKARIBISHA WAGENI |
MKURUGENZI MTENDAJI WA TANGA UWASA MHANDISI JOSHUA MGEYEKWA AKITOA MAELEZO KUHUSU UJENZI WA MRADI HUO |
MSIMAMIZI WAUJENZI WA MRADI MHANDISI FARES ARAM |
MGENI RASMI MBUNGE WA JIMBO LA MUHEZA BALOZI ADADI RAJABU |
SHEHENA YA MABOMBA YATAKAYOTANDAZWA KATIKA MRADI HUO |
MKANDARASI AKITOA MAELEZO KWA VIONGOZI WA HALMASHAURI NA TANGA UWASA |
Hassan Hashim Muheza.
Utekelezaji wa ahadi ya
Rais.
Kampuni ya Kobarg
imekabidhiwa rasmi ujenzi wa mradi wa majisafi kutoka Pongwe wilayani tanga hadi muheza ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya rais
aliyoitoa katika kijiji cha mkanyageni wakati wa ziara yake mkoani tanga.
Akizungumza katika hafla
ya kukabidhi ujenzi wa mradi huo unaosimamiwa na mamlaka ya maji safi na usafi
wa mazingira jijini Tanga mbunge wa
wilaya ya muheza Balozi Adadi Rajab amesema mradi huo wenye urefu wa kilomita
19 ni moja ya juhudi za serikali kumaliza tatizo la maji wilayani humo.
Amesema mradi huo ambao
utatekelezwa kwa kipindi cha miezi tisa ni moja kati ya miradi kadhaa ambayo
serikali imeahidi kuitekeleza.
Awali mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi jiji la
tanga mhandisi Joshua Mgeyekwa amewahakikishi wakazi wa jiji hilo kwamba hatua
ya kupeleka maji wilayani muheza haitaathiri utoaji wa huduma za Mamlaka .
Kwa upande wake mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Muheza Luiza Mlelwa amesema katika kukabiliana na
tatizo la maji halmashauri imetenga kiasi cha shilingi i 50 kwa ajili ya
kuchimba visima mia moja katika vijiji mbalimbali.
Agost 5 mwaka huu rais
John Magufuli akihutubia wananchi katika kijiji cha mkanyageni aliahidi
kushughulikia kero yamaji wilayani
muheza.
……………………………………..
No comments: