HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA WILAYA YA MUHEZA
AKINAMAMA WAKIWA KATIKA MSARAGAMBO WA KUSAFISHA ENEO LA UJENZI |
Add caption |
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA MUHEZA LUIZ MLELWA AKIMKARIBISHA MKUU WA WILAYA |
MKUU WA WILAYA YA MUHEZA MWANASHA TUMBO AKIHUTUBIA WANANCHI KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA HOSPITALI |
SIWANI WA LUSANGA AKIONGOZA AKINAMAMA KUHAMAISHA UCHANGIAJI WA HOSPITALI |
MWENYEKITI WA CCM WILAYA AKIHAMASISHA WANANCHI |
KATIBU WA CCM WILAYA YA MUHEZA MOHAMED MOYO AKIKABIDHI MCHANGO WA WA CCM MIFUKO HAMSINI KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA |
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA AKIZUNGUMZA KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA HOSPITALI YA WIALYA |
ABDULRAHMAN KITOGO MWAKILISHI WA KAMPUNI YA AGRO TANGA AMBAYO IMETOA ENEO LA EKARI 100 KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI |
Hassan Hashim Muheza.
Harambee ujenzi wa
Hospitali ya wilaya.
ZAIDI YA MILIONI 30 ZACHENGWA
Mkuu wa wilaya Muheza
Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka wananchi
Wilayani humo kujitolea
kwa hali na mali kuchangia ujenzi wa hospitali ya wilaya ili kuimarisha utoaji
huduma za afya kwa jamii.
Wito huo ameutoa katika
mkutano wa harambee na msaragambo wa kusafisha eneo la ujenzi wa hospital
ulioyofanyika katika kijiji cha Lusanga “A” wilayani hapa.
Amesema uamuzi wa ujenzi wa hospitali hiyo ambao
haujatengewa fedha katika bajeti ya mwaka huu umelenga kuboresha huduma za afya kutokana kuongezeka kwa idadi
ya watu na uhaba wa vituo vya afya hali inayosababisha msongamano katika
hospitali teule.
Akizungumza katika mkutano
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya muheza Bakari Mhando amesema ujenzi wa hospitali utawapunguzia wananchi
adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma.
atika harambee hiyo jumla
ya ahadi za shilingi milioni 30,138,000 zimetolewa mifuko 987 ya saruji mchanga
malori 162 mawe malori 60 na kokoto malori
71 ambapo mafundi mafundi 40 wamejitolea kujenga chini ya usimamizi wa mhandisi
wa wilaya ya muheza.
No comments: