HAFLA YA KUKABIDHI MSAADA WA SARUJI
MENEJA WA KIWANDA CHA SARUJI B. LEMA AKIMKABIDHI MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA MIFUKO 500 YA SARUJI KWA AJILI YA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA AFYA NA ELIMU |
MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA GULAM MUKADAM AKIZUNGUMZA MARA BAADA YA KUPOKEA MSAADA WA MIFUKO 500 YASARUJI |
KATIBU TAWALA MSAIDIZI SEKRETARIETI MKOA WA TANGA RADHIA NSUYA AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA MARTINE SHIGELA KATIKA HAFLA YA KUKABIDHI MSAA DAWA SARUJI |
Na, HASSAN HASHIM, TANGA.
Halmashauri ya manispaa
ya shinyanga imepokea msaada wa mifuko 500 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa
miundombinu katika sekta ya afya na
ujenzi wa vyoo katika shule mbalimbali wilayani humo .
Akizungumza katika hafla
ya kupokea msaada huo meya wa halmashauri Shinyanga mstahiki Gulam Mukadam amesema saruji hiyo itasaidia ukarabati wa vyumba vya
madarasa na ujenzi wa vyoo katika shule.
Amesema uboreshaji wa
sekta ya elimu ndiyo njia pekee itakayo saidia juhudi za serikali katika azma
ya kuimarisha uchumi wa viwanda .
Awali akikabidhi saruji
hiyo meneja wa kiwanda hicho mhandisi
Bernad Lema amesema wametoa msaada huo ikiwa ni kutekeleza sera ya kampuni hiyo
ya kutoa sehemu ya faida yake kwa jamii
na na kuunga mkono juhudi za serikali kuimarisha
sekta ya elimu
……………………………………………….
No comments: