TRA TANGA YAWAFUNGIA WAFANYABIASHARA WALIOLIMBIKIZA KULIPA KODI
CHUO KIKU CHA ECKENFORD |
MAAFISA WA TRA WAKIBANDIKA MATANGAZO YA KUFUNGA TANGA HOTEL |
BAADHI YA WAFANYAKAZI WA TANGA HOTEL WAKIWA WAMEPIGWA NA BUTWAA |
MAAFISA WA TRA WAKIFUNGA UTEPE KUASHIRIA KUFUNGWA KWA HOTELI HII |
Hassan Hashim Tanga.
Tra yafungia wateja wenye
madeni
Mamlaka ya mapato nchini (Tra
) mkoani Tanga imezifungia taasisi na
kampuni za Eckenford za jijini humo
baada ya kushindwa kulipa malimbikizo ya kodi mbalimbali hadi mwaka huu .
Akizungumza na waandishi
wa habari meneja wa Tra mkoa wa Tanga Masawa Masatu amesema mamlaka ya mapato imeamua
kuzifungia kuendesha biashara ikiwa ni
hatua ya kwanza ya kuwashinikiza kulipa madeni yao na kwamba endapo wa
watashindwa kufanya hivyo hatua inayofuata ni kuuzwa kwa mali zilizozouiwa.
Amesema zoezi la kufungia
taasisi na kampunini yanayodaiwa litakua
endelevu na kuwataka wafanya biashara wengine kujitokeza ili kuepuka usumbufu.
Kwa upande wake makamu mkuu
wa chuo cha Ekenford Prof John Kiango amesema yatari hatua mbalimbali zimechukuliwa
ili kuhakikisha deni hilo linalipwa katika muda uliopangwa.
Kodi inayodaiwa katika
taasisi hizo ni ongezeko la thamani (Vat) kodi inayotokana na malipo ya
wafanyakazi (PAE)na kodi ya kuendeleza
ufundi stadi (SDL) .
……………………………
No comments: