NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI JUMAA AWESO AKICHOTA MCHANGA KATIKA MRADI WA MAJI ULIOPO TUNDUMA WILAYANI MOMBA
Naibu waziri wa maji JUMAA AWESO ameagiza
shs bilioni moja zilizotolewa na Rais JOHN MAGUFULI kwa ajili
ya mradi wa maji eneo la SOGEA katika mji mdogo wa TUNDUMA
wilaya yaMOMBA mkoani SONGWE zinakamilisha mradi
huo.
Akizungumza baada ya kukagua mradi huo AWESO amesema
mkandarasi aliyepewa kujenga mradi huo kampuni ya
Best one company iwapo atashindwa
kukamilisha mradi huo kwa wakati
hawatasita kumchukulia hatua,
Amesema mkandarasi huyo akishindwa kukamilisha mradi huo
kwa muda uliopangwa
serikali haitasita kumsimamisha kazi, hali
inayochangia kero ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa eneo la SOGEA
Mkuu wa wilaya ya MOMBA
JUMA IRANDO ameitaka idara ya maji kutowapa tenda wakandarasi
wanaotuhumiwa kukwamisha juhudi za serikali za kukabiliana na tatizo la maji
Imedaiwa kuwa
baadhi ya miradi ya maji wilayani MOMBA inashindwa kukamilika kwa wakati
kutokana na uwezo mdogo wa kitaalamu wa baadhi ya wakandarasi
|
No comments: