WAHITIMU WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA.
MAANDANO YA WANAOHITIMU WA CHUO CHA UFUNDI STADI VETA TANGA |
BAADHI YA WANAFUNZI WA CHUO CHA UFUNDI VETA WAKIONYESHA UBUNIFU WA MAVAZI AINA MBALIMBALI |
KAIMU MKUU WA CHUO HAMENYA NTABAYE AKISOMA TAARIFA KWA MGENI RASMI |
MGENI RASMI KAIMU DAS SULEIMANI ZUMO AKIHUTUBIA WAHITIMU CHUO CHA UFUNDI VETA TANGA |
RAIS WA CHUO
TUMAINI SHAYO AKISOMA RISALA KWA MGENI RASMI
|
VIJANA nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za
mikopo zinazotolewa na Halimashauri nchi kwa ajili ya kujiajiri na kujiongezea
kipato badala ya kusubiri ajira za kuajiriwa .
Rai hiyo
imetolewa na kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Suleiman Zumo wakati wa
mahafali ya 41 ya chuo cha Ufundi Veta Mkoa wa Tanga
Amesema kuwa
serikali tayari imeshaweka mazingira ya
uwezeshaji kiuchumi kwa makundi ya vijana na wanawake hivyo ni jukumu la
walengwa kuja na mpango utakaoweza kuwakwamua kiuchumi.
Kwa upande
wake Kaimu Mkuu wa chuo Hamenya Ntabaye ameiomba serikali kuboresha miundombinu
ya kielimu chuoni hapo ikiwemo vifaa vya kisasa ili kuendana na kasi ya
mabadiliko ya kiteknolojia.
Ufundi stadi
ndio kimbilo la vijana wengi kwa sasa
kutokana na changamoto ya ukosefu wa ajira hivyo uwekezaji wa kimiundombinu
katika chuo hicho unahitajika kwa sasa
Jumla ya
wahitimu wapato 246 wamefanikiwa kuhitimu mafunzo yao kupitia fani mbalimbali
chuoni hapo
MWISHO
No comments: